Luke 23:26-31

26 aWalipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni mwenyeji wa Kirene, aliyekuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Isa. 27 bIdadi kubwa ya watu wakamfuata Isa, wakiwamo wanawake waliokuwa wakimlilia na kumwombolezea. 28 cIsa akawageukia, akawaambia, “Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi bali jililieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 29 dKwa maana wakati utafika mtakaposema, ‘Wamebarikiwa wanawake tasa, ambao matumbo yao hayakuzaa, wala matiti yao hayakunyonyesha!’ 30 eNdipo “ ‘wataiambia milima, “Tuangukieni!”
na vilima, “Tufunikeni!” ’

31 fKwa maana kama wamefanya hivi kwa mti mbichi, kwa mti mkavu itakuwaje?”

Copyright information for SwhKC